12/02/2004

KISA CHA JESHINI NA MENGINEYO

Samahanini sana. Siwezi kusema mengi wala kuendeleza ule mkasa wa jeshini. Mkasa huu unazidi kuwa mtamu maana Obey (tuliyemkuta kakusanya watu nje ya bweni akiwahubiria siku tunaingia Ruvu) kanikumbusha mambo kibao. Mojawapo ni ile siku tulimshikia afande Mazani mawe na kuchora chini, kisha tukamwambia, "Kama una roho ya paka ruka mstari huu!" Nimetingwa kidogo. Kabla sijakuaga nitakushauri umsikilize kwenye mtandao Nambiza Joe Tungaraza kwenye Redio Adelaide 101.5FM kila jumamosi saa nne na nusu hadi sita usiku kwa saa za Adelaide. Tunga anaendesha kipindi cha AFROWORLD. Unaweza kumsikiliza kwa kupitia mtandao wa tarakilishi. Nenda hapa. Bonyeza pahali pasemapo: LISTEN ONLINE. Tutaonana baadaye.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com