12/04/2004

SIRIKALI

Siri-kali inaweza kufanya kila kitu dhidi ya raia. Ila ambacho haiwezi kufanya ni kutuzuia KUFIKIRI. Haki ya kufikiri ni ya thamani kubwa sana. Lazima uitumie. Hakuna wa kukuzuia: sio Rais, Waziri Mkuu, FFU (Fanya Fujo Uone)...hata makasisi na mashehe hawawezi kuzuia uhuru wako wa KUFIKIRI. Ninachokushauri ni hiki: Fikiria nje ya sanduku. Fikiria nje ya mduara. Mduara, sanduku la itikadi, vyama, dini, misaafu, mfumo dume, luninga, n.k. Fumbua fumbo hili: Ukichora, chora nje ya mstari...

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com