12/04/2004

NDIMARA TEGAMBWAGE

Ndimara ni mwalimu wangu. Nimemwandikia kumwambia kuwa vijana wanauliza, "Li wapi gazeti la RADI?" Nchi inahitaji kupigwa RADI - pwa!
Nimefuma waraka ambao aliniandikia mwaka juzi. Maneno yake nimeyapenda sana. Nayaweka hapa wote tuyatafakari. Alikuwa akiongelea umuhimu wa uhuru wa kuandika:

Sasa umechokoza nyuki. Tutaandika. Tutawaandikia.Tutajiandikia. Tutajisema. Tutawasema. Tutabomoa kutaza aibu na mchoko. Tutatua "miziga" - yale magonjwayasaidiayo uzee kwa kukwamisha misuli ya miguu, mikonona hata akili. Si tunajua jinsi ya kuanza. Si sikuzote mwanzo ni HAPANA? Tunakataa tunachochukia natunafanya hivyo bila hasira wala ghadhabu. Hasira huwafupi mno. Huwa "nguvu ya soda." Sisi hutumia chukiambayo hutokana na uelewa. Ukichukia unachukua hatua.Tutakuwa pamoja katika kuchukua hatua.
Ndimara

0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com