12/03/2004

FIDELIS TUNGARAZA NA SOMO KWA WABONGO

Kufuatia kifo cha mwenzetu Charles Zawose na 'sheshe" lililozuka kutokana na roho kutu ya mama wa Kiswidi aliyemwalika kufanya kazi Uswidi, Fidelis Tungaraza kanena yafuatayo:

Ndugu Watazania wenzangu,
Marehemu Charles Zawosse , hatimaye amefika nyumbani kuzikwa kwa heshima zakibinadamu badala ya kuchomwa moto na Halmashauri ya jiji ya Stockholm.Hili ni somo kwetu wasanii na Watanzania wengine kuhuiana na hawa wageniwanaokuja kutukusanyakusanya kuja Ulaya, Marekani, na nchi zinginezilizoendelea kuwa kuna wengine na ni wengi kati yao huwa hawana utu hatakidogo. Wengi wetu tukifika huwa tunaishia kudhulumiwa na kutumikishwa bilakujua haki na vipato vyetu kamili.
Hili lililomtokea Marehemu CharlesZawosse ni moja kati ya mengi tunayokutana nayo baada ya kufika nchi zambali na ni fundisho kwetu sote.Mwanzoni mwa mwaka huu mimi pamoja na msanii mwenzangu mwingine muhitimutoka Bagamoyo tulikuwa ziarani nchi ya mbali. Tulipokuwa huko tulikutana namsanii mwenzetu muhitimu toka Chuo cha Sanaa akiwa yupo katika mpaka kati yawazimu na kujiua ambao umemkuta kutokana hawa hawa vimbelembele wanaokujakutukusanya kutuleta nchi za mbali.
Jingine kuhusu dharura ya Marehemu Charles Zawosse ni kwamba hii sera yabalozi zetu za nchi za nje kusema hazihusiki na misiba ya Watanzaniawanaokuja nchi za nje kibinafsi ni lazima ijadiliwe. Mtanzania ni Mtanzaniana ana mchango aliochangia kwenye kasha la mapato ya serikali kwa njia mojaau nyingine kwa hiyo ana hisa yake kwenye kasha la fedha za serikali ambaloanastahili kumegewa kufuatana na mahitaji yake.
Kwa mfano, Marehemu HukweZawosse baba yake Marehemu Charles Zawosse katika uhai wake alichangiamaelfu ya fedha za kigeni na za kinyumbani kwenye kasha za fedha za serikalikutokana shughuli zake za usanii. Mbali na kuchangia fedha Marehemu Hukwealijenga jina la Tanzania kiusanii duniani kote. Ninasema bila kusita kwambahakuna msanii yoyote Tanzania aliyewahi kuitangaza Tanzania kwenye mabarayote sita ya dunia isipokuwa Marehemu Hukwe Zawosse.
Mimi binafsi nilikuwepokwenye sherehe za kutunukiwa Marehemu Hukwe Zawosse Shahada ya Juu yaUdaktari wa Muziki ya Chuo Kikuu Cha Muziki cha Sibelius. Siku ya Sherehehizo bendera ya Tanzania ilipandishwa kwa heshima ya Marehemu Hukwe Zawosse!Hii ni heshima kubwa sana ambayo Watanzania wachache wanaipata kutokana namchango wao binafsi na siyo kutokana na vyeo vya kisiasa. Marehemu HukweZawosse na mwanaye Marehemu Charles walilitangaza jina la Tanzania,walitumia muziki kama nyenzo ya kutangaza hoja mbali mbali za kisiasa,kijamii na kiuchumi. Wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika ya Kusinihakuna hata onyesho moja la kimataifa ambapo Marehemu Hukwe Zawosse alikosakuuimba wimbo Mateso ambao uliaamsha fikra za kuunga mkono mapambano yaukombozi kwa mtu yoyote aliyepata kuusikia.
Huu ni mchango mkubwa sana wahali na mali ambao familia ya Zawosse umechangia kwa taifa na wanastahilikumegewa hisa kutokana na mchango wao.Kwa hayo machache anmuomba Mwenyezi Mungu amlaze Marehemu Charles kwa amani,Amen.
Ni mimi,Fidelis Mkugilo Tungaraza.

Habari ya Zawose Gazetini:
Zawose’s burial today in Bagamoyo
By James Marenga

The body of traditional jazz musician Charles Zawose, who died in Sweden amonth ago, has finally been brought back home for burial.Zawose’s young brother, Andrea Zawose told The Guardian yesterday thatfriends in Sweden topped up the family’s cash to transport their brother’sbody back home.“We have information from our Embassy in Sweden that the Swedish woman, LenaJosefsson who had a working contract with our brother didn’t contributeanything to facilitate the transportation,” he said.
He said they tried their level best to convince the woman to contribute fortheir brother’s journey but she was reluctant.Andrew said his brother would be buried in Bagamoyo today.Zawose family has accused the Swedish woman of abandoning their brother’sbody in Sweden.Charles and Lena had signed up a working contract of four years, which beganin October 12, 2004.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com