12/06/2004

WADHALIMU WAMEANZA KUTUANDAMA WANABLOGU

Kumbe wanablogu tunatisha wadhalimu namna hii. Tazama siri-kali ya jamhuri ya "kiislamu" ya Irani ilivyotia ndani wanablogu watano. Kongoli hapa. Mkina wa Kona Yangu, unaona mambo hayo? Lakini wajue kuwa tutasema na kusema na kuandika. Kama wanalinda matumbo na vitambi na akaunti zilizoko nje ya nchi, sisi tunalinda haki, ukweli, maliasili, uwazi, demokrasia na uhuru wa habari na mawazo.

Hata wafanyeje tutawashinda. Wawe na matumbi makubwa, waibe kura, waue wapiga kura kwa risasi kama ilivyotokea Dar hivi karibuni, wajenge kuta kuzunguka ikulu, watumie nguvu za dola dhidi ya mwamko wa umma...tutashinda. Nakumbuka maneno ya hayati Bob Marley katika wimbo wa Vita (War) anasema:
tunajua tutashinda,
tuna uhakika wa ushindi
wa wema dhidi ya uovu...

Hakika Ukweli na Haki vitashinda udhalimu na wizi wa mali ya wazawa nchini Tanzania na barani Afrika unaofanyika chini ya mhimili wa ubina-wizi-shaji.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com