12/06/2004

BLOGU YA KICHINA KUHUSU MAJIBWA YASHINDA MWAKA 2004

Mashindano ya kimataifa ya blogu bora zaidi yamempata mshindi kutoka China. Blogu hiyo inayozungumzia masuala ya haki za mbwa (ndio, mbwa na sio binadamu) iitwayo The Dog Newspaper imepata ushindi huo katika mashindano ambayo hujumuisha majaji wa kimataifa, nyanja 11 za blogu, ambapo kura zaidi ya 67, 000 zilipigwa kwa kila nyanja. Ushindi wa blogu hii inayozungumzia haki za wanyama unatokana na ukweli kuwa habari za wanyama hazionekani kwenye vyombo vikubwa vya habari na pia unyama dhidi ya mbwa huko China unachukuliwa kama fumbo la maisha ya wananchi huko China na mataifa mengine duniani. Nenda hapa upate uhondo kamili.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com