10/08/2005

Mabishano makali mkutano wa ConvergeSouth

Tiffany Brown amezua mjadala mkali sana. Binti huyu ambaye anablogu hapa na hapa, alikuwa akiongoza mjadala kuhusu "wanablogu wa pembezoni." Hoja yake ikiwa ni kuwa watu weusi na hasa wanawake wako nje ya mduara wa blogu ambazo zinachangia katika mijadala ya kisiasa Marekani. Dave Winer aliposikia hayo akaja juu. Tena akatishia kuondoka ndani ya chumba akisema kuwa "kama unajuka kwenye ulimwengu wa blogu acha kabisa mizigo yako huko nje...hii mambo ya mweusi, mweupe, mwanamke ni upuuzi...hii ni kinyume kabisa na nia ya blogu."
Winer akaongeza kuwa wanablogu wote wako pembezoni ndio maana wanablogu. Tumetengwa na vyombo vya habari ndio maana tunablogu...wote tuko pembezoni. Hapo ndugu mmoja akamvamia Winer na kusema kuwa wanablogu kama jamii kuna ambao wako pembezoni na wengine ni vinara.
Tiffany akasisitiza kuwa ujumbe wake ni kuwa blogu za watu weusi na hasa wanawake hazipewi kipaumbele kwenye viunganishi ndani ya blogu kubwa na hata vyombo vya habari vinapozungumzia blogu havizitaji. Akasema kuwa hazungumzii blogu zinazozumgumzia mambo kama ufumaji, upandaji maua, n.k. bali anazungumzia blogu zinazozungumzia masuala mazito ya kisiasa ambayo lazima yaingizwe katika mijadala ya kitaifa.
** Mkutano ninaozungumzia ni huu hapa.

4 Maoni Yako:

At 10/08/2005 11:04:00 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Nina uhakika huu mjadala haujaisha.Kuna ukweli ndani yake na sijui ni kwanini David anasimamisha mishipa kumpinga mwenzake.

 
At 10/09/2005 09:25:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Jeff, Wengi waliokuwa ukumbini walishangaa sana ni kitu gani kilimfanya David kuja juu namna ile. Tiffany alionyesha kwa kutumia viungo toka technorati jinsi ambavyo blogu za wanaume weupe zinavyochukua nafasi ya juu zaidi katika ulimwengu wa blogu. Na mjadala uliendelea nje na utaendelea na kuendelea...

 
At 10/09/2005 09:45:00 AM, Anonymous mshairi said...

Swala hili, kama vile Tiffany Brown anavysema, kuhusu wanablogu weupe na wanaume kuwa ndiyo wanao tajwa mahali popote litaendelea kwa muda mrefu. Lakini hata sisi wanablogu weusi (na wanawake) lazima tujisimamie. What I am saying is however much I agree with Tiffany, I really believe we should not wait for others to publicise our writings - let us aim to do it ourselves.

 
At 10/09/2005 11:46:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Kweli Mshairi, wengi walikubaliana naye kwenye hoja ya msingi ila wakasema kuwa ni jukumu la wale walio pembezoni kujiinua. wengine wakasema, "If you write good stuff, people will come to you, read you, and talk about you" hata kama wewe ni mweusi, mwanamke, n.k.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com