10/07/2005

Al Gore kwenye mkutano wa We Media

Aliyekuwa makamu wa Rais wakati wa uongozi wa Bill Clinton, Al Gore, ndiye aliyetoa hutba ya ufunguzi wa mkutano wa We Media. Ingawa Al Gore alishindwa katika jitihada zake za kuwania urais wa Marekani, hivi sasa ni "rais" wa Current TV, mradi unaoruhusu watu wa kawaida au tuseme mtu yeyote kutengeneza programu za televisheni. Katika hutba yake ya ufunguzi alisema kuwa demokrasia ya Marekani iko kwenye hatari kubwa sana. Lakini jambo kubwa zaidi ni jinsi ambavyo hakuna mtu anayeonyeshwa kushtushwa na utupu wa mfumo wa demokrasia ya Marekani.
Alisema kuwa katika mazingira ambayo zaidi ya robo tatu ya Wamarekani hadi leo hii wanaamini kuwa Saddam Hussein dniye aliyehusika na matukio ya Septemba 11, 2001 hatuwezi kuacha kukubali kuwa kuna hali ya "ajabu" katika mfumo wa demokrasia Marekani. Aliuliza: wakati nchi yetu inatesa wafungwa bila utu ni jambo la kawaida kuona hakuna Mmarekani anayeghadhabika na kuhoji tabia hii?
Alizungumzia vyombo vya habari vya Marekani ambavyo vimefanya burudani kuwa ndio habari alisema kuwa hakuna uhuru wa vyombo vya habari. Katika utafiti wa hivi karibuni, vyombo vya habari vya Marekani ilichukua nafasi ya 27 kwa kigezo cha uhuru duniani (na sio nafasi ya kwanza kama wengi tunavyodhani).
Soma hutba nzima ya Gore hapa.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com