10/02/2005

Wikipedia ya Kiswahili: Makala za msingi

Kuna ukurasa ambao unatengenezwa kwenye ile kamusi elezo ya Kiswahili. Ukurasa huu ambao ndio uko hatua za mwanzo utatoa mwanga wa aina za makala au mambo ambayo wanaopenda kuchangia wanaweza kuandika. Ukurasa huo huu hapa. Muda mfupi uliopita nimesoma ujumbe pepesi toka kwa Fide Tungaraza. Anauliza inakuwaje majina ya mihimili ya muziki wa Kiswahili haipo katika orodha ya wanamuziki tulionao kwenye kamusi hiyo? Huu ndio waraka wake: Haya, imekuwaje katika wanamuziki umewasahau Hayati Patrick Pama Balisidya, Hayati Ahmed Kipande, Hayati King Michael Enock, Mzee Kikumbi Mwanza Mpango Mwema Kiki, Mzee Makassi Kitenzogu, Bwana Ramadhani Mtoro Ongala, Bati Osenga Ipopolipo, Mzee David Mussa, Cosmas Thobias Chidumule, Mzee Luza Elias, Mzee Kassim Mapili, Mzee Juma Ubao, Mzee Muhidin Mwalimu Gurumo(Chongo), Mzee Kassim Mabela...
Kwanza lazima nikiri kuwa Fide ana kumbukumbu. Kawataja wanamuziki hawa majina yao yote hadi yale ya utoto. Kamkumbuka hadi Bati Osenga. Pili, napenda kusema kuwa majina ya watu, vitu, nch, chochote kile kilichopo katika kamusi elezo hii ni hatua tu ya mwanzo.
Tatu na muhimu ni kuwa iwapo kuna jambo unaona linafaa kuwekwa na haliko au kuna jambo la kubadili/kurekebisha mtu yeyote anakaribishwa kufanya hivyo. Ndio faida ya teknolojia ya "wiki" ambayo inawezesha watu kufanya kazi hii ya kuandika kamusi elezo kwa mantiki ya kijamaa. Sasa huu ni ujamaa au unabisha?

2 Maoni Yako:

At 10/06/2005 01:49:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Nimekumbuka kwamba niliwasahahu magwiji wa taarabu kina Hayati Mzee Issa Matona, Mzee Bia Hassan, Mzee Khamis Shehe, Bwana Ilyasi Mohamed, Hayati Siti Bint Saad, Bi Shakila Mohamed, Bi Elizabeth Sijila, Bi Patricia Hiraly, Bi Mwapombe Hassani na Bwana Sami Dau(Waimbaji original wa ile classic ya kudumu Subharkeri Mpenzi, kwa sasa hivi hao ndiyo walionijia kichwani lakini nikirudi nyumbani nitatazama kwenye maktaba yangu nikuletee orodha ndefu zaidi. Pia katika muziki wa dansi nadhani niliwasahau kina Hayati Kinyonga wa Simba Wanyika na Hayati Professor Omar (mtungaji mwenza wa ile ya classic nyingine ya kudumu Sina makosa). Pia Bwana John Ngereza wa Les Wanyika, Zahir Ali Zorro wa JKT Jazz, Mzee Shem Kalenga wa Tabora Jazz (mtunzi wa classic nyingine ya kudumu Nyumbani kwao Wamezidi ukali) James Mpungu(Mtunzi wa Ihepi krismasi hiyo hiyoo) Nitaanza shughuli za kuandika wasifu wa wanamuziki katika hii kamusi hivi karibuni bado naendelea kukusanya maelezo zaidi.
Mapambano yanaendelea,
Ni Mimi Fidelis 'Mti Mkubwa' Tungaraza.

At 10/06/2005 02:11:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com