9/27/2005

Nitakwenda Mkutano wa ConvergeSouth na Pop!Tech

Nitakapomaliza mkutano wa We Media: Behold the Power of Us kule New York tarehe 5 mwezi ujao, nitaondoka nikikimbia nikikatiza "shotikati" moja ya kupitia kwenye mashamba ya mahindi kuelekea North Carolina kwa ajili ya mkutano mwingine mkubwa kuhusu zana mpya za mawasiliano (masuala ya blogu yakiwa yamepewa kipaumbele) utakaofanyika tarehe 7 na 8 mwezi ujao katika chuo kikuu cha A and T, North Carolina. Mkutano huu utakaomshirikisha mwanablogu anayesukuma vuguvugu la kidemokrasia nchini Irani kwa kutumia blogu, Hoder, unaitwa ConvergeSouth. Kisha tarehe 19-22 mwezi Oktoba nitakuwa katika mji wa kizamani wa Camden katika jimbo la Maine kuhudhuria mkutano wa kila mwaka unaokutanisha watu toka sekta mbalimbali kujadili na kubadilishana mawazo juu ya teknolojia na mabadiliko ya jamii. Mkutano huu unaitwa Pop!Tech 2005.


1 Maoni Yako:

At 9/27/2005 04:47:00 AM, Blogger Hector John Mongi said...

Kila la Heri kaka! Mwanaharakati lazima ajue kukimbia mhakamhaka na pia vijia vya mkatizo na vichochoro. Tunatarajia mrejesho kutoka katika mikutano hiyo. Pia usisahau GUMZO

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com