9/11/2005

Helsinki: Mtengeneza Filamu anayetetea Waislamu

Mmoja wa washiriki wa mkutano wa Helsinki, Naeem Mohaiemen, alisema jambo ambalo limekuwa midomoni mwa wajumbe toka alipozungumza. Naeem ambaye ni mtengeneza filamu (bofya hapa uone moja ya filamu zake) alidai kuwa wakati ambapo mkutano huu nia yake ni kuunganisha washika dau mbalimbali ili kuweza kujenga demokrasia na usawa sauti za waislamu zimesahaulika. Alisema kuwa kutokana na mtazamo wa watu wengi duniani kuhusu waislamu na uislamu ni vyema waislamu wakahusishwa kikamilifu katika miradi kama hii. Pia alitaka wasanii nao kuhusishwa zaidi kwani wao wana uwezo mkubwa wa kushawishi na kuelimisha umma kutokana na kazi zao.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com