9/09/2005

KUNA RISASI MBILI KWA KILA KICHWA DUNIANI

Katibu Mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, Irene Khan, akiongea hapa Helsinki jana, alisema kuwa vita dhidi ya ugaidi vimekuwa ni kisingizio cha baadhi ya nchi duniani kutupilia mbali haki za msingi za binadamu.
Akizungumzia kuhusu vita duniani alisema kuwa silaha ndogo ndogo, ambazo ndio zinazotumika katika vita sehemu mbalimbali duniani, ndio hasa silaha za maangamizi. Mataifa makubwa yanayopata faida kubwa kutokana na biashara ya silaha hizo lazima yabanwe ili kuacha biashara hiyo chafu. Zaidi ya watu nusu milioni huuliwa na silaha ndogondogo kila mwaka.
Alimaliza kwa kutuambia kuwa idadi ya risasi zilizoko duniani ni kubwa mno kwani kuna risasi mbili kwa kila binadamu hapa duniani.

1 Maoni Yako:

At 9/09/2005 08:00:00 AM, Anonymous oscar munishi said...

kweli mr ndesanjo nimeshtushwa sana na habari hii ya kila kichwa cha mwanadamu mmoja kimewekewa au kimetengewa risari mbili.hii hali inatisha sana.
naomba wote tujiulize "je risasi hizo zimetengenezwa kwa sababu ya nani na kwa nini?"
hapo ndipo utajua mwanadamu ni katili sana hasa kwa mwanadam mwenzake,na pia ndio tutaweza kugundua kwa nini kuna uvamizi wa nchi nyingine kwa kisingizio cha ugaidi! au utengenezwaji wa silaha za nyuklia!au tunatafuta mahata pa kufanyia majaribio silaha zetu?
naomba niache swali kwa watu wote, je nini kifanyike ili kushinikiza haya mataifa kuacha au angalau kupunguza utengenezwaji wa silaha hizo?
ndesanjo,padre Karugendo,Mihangwa nanyi waandishi wengine tunawategemea sana katika kupambana na kulifunua hili la silaha kwa jamii yote kuwa si sawa,tunategemea mtueleze athari za kumiliki silaha kwa wingi,na tunaomba mtueleze kwa upana sana kuhusu kifanyike nini ili kupunguza uzalishwaji wa silaha.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com