9/05/2005

Tovuti za habari za uchaguzi Tanzania

Tayari wameanza kuzunguka huku na kule. Wauza maneno. Wamebeba mabakuli, vikapu, makopo, viroba, n.k. vilivyojaa hadithi tamu tamu. Mwaka huu ukikosa ubwabwa, basi usikose fulana. Ukikosa fulana, jitahidi usikose mshiko. Ukikosa mshiko basi lazima upate udirinki kwenye viti virefu.
Ndio, uza nchi na utu wako kwa sahani ya ukoko wa ubwabwa. Hapana, akikupa ukoko usimpigie kura...hadi akupe utando.
Ndio umefika ule wakati. Tazama tovuti ya Kura Yako na Uchaguzi Tanzania kwa habari za mchezo huu wa kuigiza utakaofikia kilele chake mwezi wa kumi.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com