9/02/2005

Nakwenda Helsinki

Jumatatu ijayo ninaondoka kwenda kwa Wafini (nchini Finland). Nitakuwa katika jiji la Helsinki kushiriki na kublogu mkutano wa Helsinki 2005 kupitia mradi wa Sauti ya Dunia na Wizara ya Mambo ya Nje ya huko Ufini.. Kwa kuwa mkutano huo unahudhuriwa na rais anayemaliza muda wake na pia rais ajaye wa Tanzania, huenda nikapata nafasi ya kunywa nao kahawa kujadili "maendeleo" ya nchi.

Hivi sasa ninajisomea mambo mawili matatu kuhusu nchi hii. Mwandani, asante kwa simu ya "meya" wa jiji la Helsinki.

Nitaandika zaidi juu ya safari hii.

3 Maoni Yako:

At 9/03/2005 03:32:00 AM, Blogger Rama Msangi said...

Waambie kuwa sisi tumechoshwa na huu utaratibu wao wa kutung'onga. Hivi unajua wanaposema CCM Hoyeeeee ndani ya nafsi zao wanaanisha nini hasa kaka?? Wanachomaanisha ni SISI KWA SISI OYEEEEEE! yaani wao kwa wao sasa hayo mambo na unafiki huo hatuutaki nadhani pia itakuwa fursa nzuri huyu jamaa akueleze kuwa kasi yake ni ya kuelekea wapi hasa asiache kauli mbiu yake inaelea tu maana kama nilivyosema kukimbia bwana sio lazima kwenda mbele ati

 
At 9/03/2005 09:00:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Kila la heri na safari yako, mi sielewi hao waheshimiwa wanapohudhuria mikutano kama hiyo na wanaporudi nchini mwao wana "apply" miundo-mbinu gani waliopata na hata pale wanaposhauriwa kuhusu "maendeleo" na mtu yeyote sielewi kwa nini hawako tayari kuwajibika. Na kuwajibika huku si lazima wafanye walichosikia au kushauriwa ni kufanya hata upembuzi yakinifu ili waone kama watakapo "apply" huo muundo-mbinu utaweza kuleta matunda gani. Kweli sijui ni nani pale Tanzania anatakiwa apewe muundo-mbinu/ushauri endelevu ambao utatusaidia sisi wote kama nchi, nimezaliwa huko Tanzania ila hili swala siku zinavyozidi kwenda nashindwa kujua ni nani mhusika "Mkuu"....

 
At 9/03/2005 10:06:00 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Safari njema Macha.Nina uhakika utakayoyapata huko utatumegea na sisi kupitia hii njia rahisi ya mawasiliano ya umma.Kila la kheri

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com