9/01/2005

Nini Tofauti ya Kuiba na Kuchukua Kisicho Chako?

Tofauti ya kuiba na kuchukua ni hii: watu weusi ndio huiba na weupe huchukua!
Maafa ya kimbunga cha Katrina hayaelezeki. Wakati maafa haya yakitawala vyombo vya habari kuna habari moja ambayo huenda imekupita. Habari hiyo ni kuhusu picha mbili ambazo zimezua mjadala kwenye mtandao wa kompyuta. Picha moja, hii hapa, inamuonyesha kijana mweusi akiwa na bidhaa kadhaa. Maelezo ya picha hiyo yanaonyesha kuwa huyu kijana katoka kuiba kwenye grosari moja. Picha nyingine, hii hapa, inaonyeshwa watu weupe wawili, nao wakiwa "wamechukua" mikate na soda toka kwenye grosari moja. Ila maelezo ya picha hii hayasemi kuwa wameiba. Tunaambiwa kuwa wamebeba mikate na soda "waliyoikuta" kwenye duka moja. Kwa maneno mengine hawa weupe hawakuiba bali walichukua. Ila yule mweusi ameiba!
Sasa mjadala huu umepelekea jamaa wa Yahoo! kuondoa picha hiyo ya watu weupe. Halafu wametoa tamko hili. Ajabu ni kuwa ile ya mweusi "aliyeiba" imeachwa. Wameona kuliko kubadili maneno na kusema kuwa wale weupe nao wameiba ni afadhali waitoe ile ya weupe na kuacha ya jamaa weusi "wezi."

1 Maoni Yako:

At 9/02/2005 12:25:00 AM, Blogger Egidio Ndabagoye said...

Huku watu wengi wanajiuliza hivi katika majimbo yaliyopigwa na Katrina hakuna wazungu sababu picha za televisheni zinaonyesha watu weusi tu ndio walio katika matatizo:hawana chakula,sehemu za kulala...

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com