9/08/2005

Watanzania wanaohudhuria mkutano hapa Helsinki


Muhidin Issa Michuzi kamaliza kutuchukua picha hii. Hawa wote ni Watanzania wanaohudhuria
mkutano hapa Helsinki. Kutoka kushoto ni ndesanjo mwenyewe, Abubakar Rajab ambaye ni katibu mkuu wizara ya kazi na maendeleo ya vijana, Philipina Labia wa shirika la Faraja Human Development Trust Dodoma na mjumbe wa bodi ya TANGO, Halima Zinga wa Chama cha Elimu ya Watu Wazima Tanzania, Angel Damas wa Youth of the United Nation Association (ambaye ndiye miss Tanzania 2005), Abdulkader Shareef (Naibu Waziri, wizara ya mambo ya nje), Felista Rugambwa wa Youth of the United Nations Association (ambaye ni Miss University 2005), anayefuata nitatafuta jina lake, Omary Mjenga wa wizara ya mambo ya nje, na Robert Kahedaguza toka wizara ya mambo ya nje, anayefuata nimemsahau jina ila katoka maendeleo ya jamii

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com