HELSINKI: MALAIKA NAKUPENDA MALAIKA
Jana nilisahau kuelezea jinsi Watanzania "tulivyowakilisha" kwenye tamasha la kufunga mkutano wa Helsinki. Wakati watumbuizaji kadhaa wa hapa Finland wanafanya vitu vyao, Mama Maria Shaba, mwenyekiti wa Tango, alikujanje ya ukumbi kutubeba mkikimkiki. Kisa? Alisema lazima Watanzania tukatumbuize. Da! Sauti tunazo? Akasema lazima. Basi Watanzania wote hao jukwaani. Mama Shaba akashika kipaza sauti na kutambulisha kundi la muziki la Tanzania likiongozwa naye akiwa na sauti ya kwanza na Muhidini Issa Michuzi sauti ya nne. Mimi sauti yangu sijui wala ni ya ngapi. Basi tukashusha Malaika nakupenda malaika huku tukijinesuanesua. Ukumbi ukabaki mdomo wazi, waliokuwa mbali wakasogea karibu, mtu wa taa akazitengeneza vyema, zikatumulika. Tukaimba. Tukawakilisha. Tukashangiliwa. Tukafurahi.
Tulipomaliza malaika ikawa sio mwisho. Tukaondoka ukumbini huku tukiimbisha watu wote kiitikio cha wimbo wa Bob Marley wa Get Up Stand Up....Stand Up for Your Rights....come one everybody...Get Up Stand Up....huku tumenyoosha mkono uliokuja ngumi hewani.
1 Maoni Yako:
Kaaaaaaaaazi kwel-kwel!!
Post a Comment
<< Home