9/27/2005

Huenda Niko Karibu Nawe

Baada ya kuondoka kwenye ule mkutano wa kuuziana maneno kama ilivyo mikutano mingi niliingia mitini kimya kimya. Nilikwenda mahala kwa mapumziko kisha nikaenda kwa Kichaka. Kisha nikaondoka tena, kimya kimya. Sasa niko mahala fulani ambapo sipendi kusema ni wapi! Lakini utashangaa...huenda niko jirani nawe. Huenda niko mtaa wa pili na hapo ulipo. Kwahiyo tukikutana barabarani, kijiweni, au mgahawani usije sema sikukwambia. Huenda niko Aruba. Au labda visiwa vya mtakatifu Helena. Au pengine niko pembeni ya kwa msikiti wa Kwa Mtoro jijini Dasalama. Au labda pembeni ya soko la Kiboriloni mjini Moshi. Au ufukweni mwa bahari Mambasa (yaani Mombasa). Au kwa Bibi Lizabeti. Au Trenchtown kwa Bob Malya, nchini Jamaika. Utajaza mwenyewe.
Nilipo ninavaa miwani nyeusi kila siku. Na kichwani kofia kubwa. Unaweza usinitambue. Jaribu kutafuta mtu mwenye miwani nyeusi ya ki-KGB na kofia kubwa ambaye anatembea na kompyuta ndogo ya mapajani akitafuta mawimbi ya mtandao usiwaya (wi-fi). Ni mimi.
Nina picha tulizopiga pale klabu ya Chelsea, jijini Helsinki. Hapa ndio wanapokutana Watanzania wanaoishi Helsinki. Basi wageni na wenyeji tulikutana hapo na kupiga picha. Kabla sijazitundika nitawauliza kwanza walioko kwenye picha kama ni sawa kuziweka hapa.

2 Maoni Yako:

At 9/28/2005 05:08:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Kama hauko gleneagles basi uko helsinki, huenda nimekuona au yule amekuona. najua rangi ya ngozi yako na urefu wa nywele zako, wengine pia wanajua.
Labda uwe unatoka usiku tu kama mwizi wa zamani, siku hizi kuna wezi hadi mchanamchana,sijui kama wanaogopa au wanapenda kuchomwa moto maana wanazidi kuongezeka lakini mie kaa, bora nilipwe 5000/= kwa wiki inatosha.
Ukijificha mithili ya mwizi tutakufichua kama tunavyofichua wezi watoto,huna madaraka hivyo huwezi kuwa mwizi mkubwa tushindwe kukufichua.
Karibu yangu nao wanacheza salama sijui upo karibu kiasi gani lakini wasafiri ni wengi na kila pembe ya dunia hivyo cheza salama lakini usikaribie sana nitakuona.
Mloyi.

 
At 9/29/2005 03:17:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Bw. Macha,
Salaam.
Nashukuru kwa kutuhabarisha kuhusu matukio mbalimbali kwa kupiti akwenye blog yako.
Mimi nasubiri kwa hamu hizo picha mlizopiga kwenye club ya Chelsea ulipokuwa nchini Finland.
Natanguliza shukrani.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com