9/11/2005

Helsinki: Rushwa na Maendeleo

Kati ya mijadala iliyokuwa mikali ni ule kuhusu rushwana maendeleo. Ilikubalika kuwa moja ya chanzo kikubwa cha rushwa katika jamii mbalimbali duniani ni rushwa. Ami Mpungwe wa Namitech East Africa alidai kuwa tofauti na mtazamo wa wengi rushwa sio tatizo la nchi masikini tu. "Tatizo ni kuwa rushwa ikitokea nchi tajiri inaitwa kashfa, ikitokea nchi masikini inaitwa rushwa," alisema.

Naye Waziri wa Serikali za Mitaa wa Kenya Musikari Kombo alidai kuwa tatizo kubwa kwa nchi za Afrika ni kuwa fedha zinazopatikana kwa rushwa Afrika hupewa sehemu ya kuhifadhiwa katika nchi tajiri.

Naye Birgit Errath wa Global Compact akiongea nami kwenye mahojiano kuhusu rushwa alisema kuwa dunia inapoteza kiasi cha cha dola zisizopungua trilioni moja kwa mwaka kutokana na rushwa.

Nini hasa dawa ya rushwa?

2 Maoni Yako:

At 9/12/2005 09:30:00 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Ndesanjo,
Napata kizunguzungu ninaposikia kwamba washika dau kama Ami Mpungwe ndio vinara wa kuiongelea "rushwa"

 
At 9/23/2005 01:00:00 AM, Blogger Martha Mtangoo said...

Haki ya Mungu suala la rushwa bado ni kitendawili kabisa hapa kwetu Tanzania Rushwa imehalishwa na sasa inatwa Takrima hapo ndipo ninapochangikiwa na hili suala la RUSHWA, TAKRIMA, KASHFA NA mambo mengine yanayofanana na hayo anyway hapa cha msingi ni lazima tukubaliane kuwa Rushwa kamwe haiwezi kumalizika nafikiri hii ni laana ambayo kuisha kwake ni sawa na kumpigia Kiziwi Mziki mkubwaa wakati hasikii!!!!!!!!!!

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com