9/27/2005

Usikose Mahojiano Kuhusu Kiongozi cha Wanablogu Leo

Mambo mengi yametokea na yanaendelea kutokea toka niandike mara ya mwisho. Yapo ambayo nisingependa yakupite. Kwanza kabisa leo hii kutakuwa mahojiano kati ya mkurugenzi wa masuala ya mtandao wa Wanahabari Wasio na Mipaka, Julien Pain, kuhusu kitabu kizuri sana walichokitoa kuhusu uanaharakati wa mtandaoni. Kitabu hiki ambacho ni kiongozi cha wanablogu na wanaharakati wa mtandaoni kinapatikana bure hapa. Mtu yeyote anaweza kushiriki kwenye mahojiano hayo ambayo yatafanyika kwa kutumia teknolojia ya Internet Relay Chat (IRC). Taarifa kamili kuhusu saa na jinsi ya kuingia kwenye mtandao huo wa IRC nenda hapa.

Rebecca MacKinnon amechambua kwa ufupi yaliyomo katika kiongozi hiki. Msome hapa.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com