9/28/2005

Wikipedia Ya Kiswahili

Ile kamusi elezo ya Kiswahili (Kiswahili wikipedia) ambayo inaandikwa na kuhaririwa na mtu yeyote anayezungumza Kiswahili inahitaji msaada wako wewe mpenda lugha yetu tamu...kumbuka Shaban Robert na "titi la mama litamu ingawa la mbwa..." Kamusi hii ukilinganisha na kamusi elezo za lugha nyingine kama vile wikipedia ya kiingereza , kifaransa au Kidachi iko nyuma kidogo. Yeyote yule ambaye ana muda anaweza kushirika kuipanua kwa kufanya mambo kadhaa: kuandika makala mpya, kuhariri zilizopo, kuitangaza (hawa wanablogu wana nafasi ya kuitangaza), n.k. Ukienda hapa utapata taarifa zaidi juu ya mambo ya kufanya ili kuiboresha. Ukurasa mkuu wa wikipedia yetu huu hapa.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com