10/02/2005

Blogu ya Gikuyu imetinga uwanjani

Rafiki yangu Gatua wa Mbugwa, ambaye niliwahi kuitangaza CD yake ya mashairi ya Gikuyu, ameanza kublogu kwa lugha ya Gikuyu akiwa na nia ya kuendeleza na kuenzi utamaduni wake. Gatua hivi sasa anasoma shahada ya udakitari nchini Marekani. Kama alivyofanya wakati akiandika tasnifu yake ya shahada ya pili katika chuo kikuu cha Cornell, tasnifu yake ya udakitari ataiandika kwa Gikuyu! Hongera Mbugwa wanablogu twakukaribisha. Mtembelee hapa na kumkaribisha hata kama huongei Gikuyu.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com