10/02/2005

Isiwe tabu...pilau hata nyumbani nitakula

Mwanablogu Ahmed wa Saudi Arabia anatupasha kupitia blogu wa Sauti za Dunia (Global Voices) kuhusu mwanablogu Al-Farhan aliyeamua kuondoka katika tafrija maalum ya "mpiga tarumbeta" wa Joji Kichaka, Karen Hughes, huko Saudi Arabia. Jamaa alikereka na kitendo cha kuwepo kwa wanawake wengi na watu wenye siasa za kiliberali katika tafrija hiyo. Kabla hajatia chakula mdomoni akaamua kunyanyuka na kuondoka za. "Ya nini bwana...kwani hiyo pilau hata nyumbani si naweza kula?" Akajisemea. Soma kisa chote hapa.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com