10/04/2005

Waraka wa kampeni ya Mnyika

Mkurugenzi wa Vijana wa Chadema, ndugu John Mnyinka, akichaguliwa kuingia bungeni mwaka huu huenda atakuwa mbunge kijana kuliko wote. Hivi sasa ana miaka 24. Ndugu Alex Mayunga kanitumia waraka huu akimpigia kampeni mwana Chadema huyo. Ujumbe wa Mayunga huu hapa chini:

Ndg, zimesalia siku chache kabla ya kuifikia nchi ya ahadi, ahadi ambayo hatukuitiwa ila tumeitika...naam kwenye asali na maziwa...30 0ktoba 2005 tutamchagua JJ Mnyika awe Mbunge wa Ubungo....Mnyika hatoweza kuwa Mbunge kama wewe na wale marafiki zako watano hawatawaambia wenzao watano ili waongee na wenzao watano...mnyororo ni mrefu kwa kweli...watumie tafadhali....tunahitaji kulikomboa jimbo hili.

1 Maoni Yako:

At 10/06/2005 01:45:00 AM, Blogger mloyi said...

Asali na maziwa sio Nyuki na fahari lenye kichaa.
Ndiyo, hataweza kuwa mbunge kama mimi na wenzangu watano wasipompigia kura.
Hata nchi haitakuwa na usawa kama mimi na wewe hatuta ongelea rushwa waziwazi na kuikana kama tulivyomkana shetani na mambo yake yote.
Tunahitaji vijana bungeni wawe ni vijana shupavu wapigania wanyonge kama kipenzi cha vijana ulimwenguni, che guevera.
Tunahitaji kulikomboa jimbo hili, ungeongelea familia hii ingekuwa nzuri zaidi.Na kuziacha familia nyingine hazina huduma za msingi.
Mwezi mzima sasa hatufanyi shughuli yeyote isipokuwa kusikiliza hoja za watu wasioisha, leo Mrema kesho Mbowe, mara kikwete na wengine nisiokumbuka majina yao.
Tuambie kitu cha ukweli tutakusikiliza.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com