10/02/2005

Kibira aja na filamu ya TUSAMEHE

Ndugu yetu Josiah Kibira anayeishi kwa Joji Kichaka ametoa filamu nyingine kigongo. Kigongo chake cha kwanza wengi walikivulia kofia. Kigongo hicho kilikuwa ni ile filamu ya Bongoland. Filamu hiyo ambayo ilikuwa ya Kiswahili ikiwa na maandishi ya chini ya picha kwa kiingereza imependwa na kila aliyeitazama hasa kwa jinsi ilivyoonyesha masahibu ya kuinga mtoni. Filamu yake hii mpya ya Tusamehe inahusu janga la Ukimwi. Itaanza kuonyeshwa rasmi mwezi nchini Marekani na baadaye kupelekwa Afrika. Soma zaidi juu ya Tusamehe hapa.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com