10/08/2005

Jimmy Wales wa Wikipedia na Ruby wa Lotus Media

Jana usiku wakati wa tafrija nyumbani kwa David na Jinn, niliweza kukaa na kuongea na Jimmy Wales. Jimmy ni mkurugenzi wa Wikimedia Foundation na mwanzilishi wa mradi wa Wikipedia ambao unajumuisha ile kamusi elezo (Kiswahili wikipedia) ya Kiswahili. Moja ya mambo tuliyoongea na mbinu zinazoweza kutusaidia wazungumzaji wa Kiswahili kupanua kamusi yetu. Jimmy alisema kuwa hivi sasa anatafuta wafadhili ili kuweza kupata fedha za kupanua na kuongeza ushiriki wa wazungumzaji wa kiswahili katika kutengeneza kamusi elezo ya Kiswahili.
Zaidi juu ya Jimmy tazama hapa.
Muda mfupi uliopita nilikuwa naongea na Ruby ambaye ataanza kuongea muda sio mrefu kuhusu matumizi ya Intaneti kwenye harakati za kisiasa. Ruby ndiye muhusika wa Lotus Media. Tazama hapa.
Kwa kukumbusha ni kuwa ninahudhuria mkutano wa ConvergeSouth. Ratiba ya leo hii hapa.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com