10/08/2005

Mabishano Makali - 2

Niliandika hapo awali juu ya mabishano makali wakati wakati Tiffany Brown alipokuwa akiongelea suala la baadhi ya wanablogu, kwa mfano wanawake weusi kuwa pembezoni. Kama hukusoma niliyoandika yasome hapa kisha ndio uendelee. Sikumaliza kuelezea kisa chote. Basi wakati fulani mabishano yalivyozidi kuwa makali, David akiwa anaongelea suala fulani akasema, "Nasoma wanablogu wanawake..." Nikakurupuka bila kunyoosha mkono na kumuuliza, "kwanini unawaita hao wanablogu wanawake?" Akatoa majibu ya hapa na pale, nikamkatiza kabla hajamaliza na kurudia swali langu. Sababu ya kumuuliza hivyo ni kutokana na yeye kusema kuwa kwenye masuala ya blogu hakuna haja ya kuanza kusema huyu ni mwanamke, huyu ni mweupe, n.k. Sasa ndio nikamshangaa kwanini anazungumzia wanablogu kwa kutaja jinsia yao?
Baadaye mzozo ukiwa ndio unawaka moto zaidi, mwanamama mmoja akamwambia David, "Sina nia ya kukutukana ila najua u karibu kustaafu..." We! David alikuja juu hasa. "Huku ni kutukana. Ndio mambo haya ya kutazama watu na kudhani unawafahamu. Mimi hunijui. Unawezaje kusema eti karibu nistaafu?"
We!
Haya, nakwenda kwenye somo kuhusu teknolojia ya podikasiti.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com