10/11/2005

Blogu Mpya ya Motowaka ya Ndugu Mloyi

Mshikaji Mloyi ni kati ya watu ambao barua zao pepe wanazonitumia huwa kama vile nasoma riwaya fulani. Nimefurahi kuwa amenza kublogu. Na hili ni shairi aliniandikia akinitaarifu juu ya blogu yake hiyo:

Karibuni nawaalika,
sijui nitaishi mpaka lini,
kifo kikinipata,
nitashukuru kwa mazuriyangu,
Mabaya yotenitaomba niende nayo,
karibuni kwangu,
naomba pawe pazuri,
nyuki wangurumena maua yachanue,
vipepeo wajae kama tutamaniko kwenda sote,
kaibuni kwangu kwa wingi mjongee,
maisha marefu naombea,
nyumba yangu imepata jina,
itawasha moto wa heri,
motowaka ndilo jinale.
blogspot mbeba wake,
karibu motowaka.blogspot.com,
kibarazani kwake kuna heri
hakuna wacheza kamari,
na hata karata tatu,
upatu nao hauruhusiwi.
karibuni kwa heri,
hapa shwari hamna shari.
***************************

Soma hapa chini moja ya barua zake pepe ninazozungumzia:

Huku tumezoea wagombea uraisi wa maisha, sasa pia wapo wabunge wa maisha wanaong'ang'ania ubunge kama vile ndiyo dawa ya kifo...wengine kuambiwa na wananchi ubunge basi, wameasi kauli zao zote za kidumu chama cha mapinduzi!!! na kuhamia vyama vya upinzani. Nipe kura yako nami nitakuletea maendeleo! labda maendeleo toka mbinguni, sijui, wao wanaweza kuwa watakatifu wenye roho nyeupe kama theluji na wapendwa wa bwana hivyo wataweza kumshauri mungu amalize umasikini alioukodolea macho ukue tangu siku alipoumba dunia hadi sasa umekithiri!
Sala zote za watu wa mungu hazijawahi kusikilizwa leo kuna mkombozi anayedai anaweza kuzuia umasikini kwa kushirikiana na IMF. Labda kwanza mungu awe mwehu au alale usingizi.
Haya blogu ya Mloyi hii hapa.

2 Maoni Yako:

At 10/12/2005 02:16:00 AM, Blogger Indya Nkya said...

Macha huyu bwana ananifurahisha sana. Anaandika vizuri kweli. Nimefurahi kwamba ameingia kwenye huu ukumbi wa kupashana habari kwa njia ya blogu

 
At 10/13/2005 12:48:00 AM, Blogger mloyi said...

asante kwa kunipigia kampeni. Nitajitahidi kampeni zako zisiwe za uongouongo. hata jua lichomoze saa tatu usiku.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com