3/25/2005

"UONGO HUO" - JHIKO MAN

Rafiki yangu Da' (unajijua) umenitajia Jhiko Manyika. Nimemsikiliza sana leo. Kuna nyimbo zake mbili nadhani lazima azirekodi tena. Hasa wimbo wa Uongo huo. Leo nimeusikiliza vizuri sana. Nitawapigieni hapa siku moja. Ngoja niwapeni maneno ya wimbo huo. Kabla sijawapa, kwa wasiomjua, Jhiko Manyika ni mwanamuziki wa Rege nchini Tanzania. Tazama picha yake hapa.

UONGO HUO

Uongo huo, uongo huo, uongo huo,
Tusisumbukie uongo
Tuijue kweli na hiyo kweli
Itatuweka huru

Wale Waafrika tusio makini
Tumedanganyika,
Wakati ndugu zetu wanadai utu wetu
Sisi tunalalamika,
Wale Waafrika tusio makini
Tumedanganyika,
Wakati ndugu zetu wanadai utu wetu
Sisi tunakasirika

Tamaduni zetu
Tunasema ni za kishenzi,
Wazee wa kuwapa heshima
Tunasema ni wachawi wanatuua

Uongo huo, uongo huo, uongo huo,
Tusisumbukie uongo
Tuijue kweli na hiyo kweli
Itatuweka huru


Wale Waafrika tusio makini
Tumedanganyika,
Wakati ndugu zetu wanadai utu wetu
Sisi tunalalama,
Wale Waafrika tusio makini
Tumedanganyika,
Wakati ndugu zetu wanadai utu wetu
Sisi tunalalamika


Tunathamini vitu
Tunasahau utu

Uongo huo, uongo huo...

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com