3/24/2005

MAPINDUZI YA UMMA AU ?

Kwa sasa siwezi kujua kama haya ni mapinduzi ya umma kwa faida ya umma au ni mchezo wa kuondoa wezi hawa na kuingiza wezi wale. Imetokea leo hii huko Kyrgyzstani. Historia ya mapinduzi kama haya ni ndefu. Kwa miaka ya karibuni tuna mifano michache. Yalitokea kule Jojia. Kongoli hapa. Kisha tukasikia Ukraine nako. Hapa. Halafu ikaja zamu ya Lebanoni. Hapa. Na sasa imetokea Kyrgyzstani. Hapa. Baadaye itakuwa wapi? Swali ninalojiuliza ni hili: mapinduzi haya ni kwa faida ya nani? Kitendo cha Marekani kushabikia mapinduzi ya Ukraine na kule Lebanoni kinafanya watu wengi wasite kufurahia kuwa umma umetwaa madaraka toka mikononi mwa wezi wachache. Tuna macho, tuna akili, tusubiri. Jambo la kushukuru katika yote haya ni kuwa hakuna watu walionyanyua silaha na kuingia msituni.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com