7/23/2004

Wanablogu ni Waandishi?

Bado mjadala huu haujatuama. Je wanablogu (bloggers) ni waandishi wa habari? Je blogu ni uandishi? Waandishi, wanasiasa, watengeneza sera, wanataaluma, n.k. wana mawazo tofauti juu ya blogu. Wako wanaosema kuwa wanablogu (bloggers) ni aina fulani ya waandishi. Wengine wanasema hapana. Lakini kukubaliwa kwa wanablogu kuhudhuria mkutano wa chama cha Demokrasia cha hapa Marikani, ambao utampitisha John Kerry na John Edwards kuwa wagombea Urais na mgombea mwenza, kumechukuliwa kama ni moja ya hatua ambazo zinawapa wanablogu hadhi ya uandishi.

1 Maoni Yako:

At 7/26/2004 12:22:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Wana blogu ni akina nani?

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com