7/20/2004

Yesu Anakuja!

Bado ninaendelea kukumbana na watu wanaohubiri kuwa Yesu yu karibu kuja. Mimi siwaelewi kabisa. Ninavyoelewa mimi ni kuwa Yesu yu karibu aondoke. Yuko nasi toka siku nyingi ila hatujui. Sijui tunasubiri ashuke toka mawinguni. Unajua asilimia 90 ya mambo ambayo Yesu aliyasema yalikuwa ni mafumbo. Usipoweza kufumbua, utabaki ukimsubiri. Kwanza watu wengi wanaomhubiri Yesu, hawamfahamu Yesu sawasawa. Yesu ninayemjua mimi akija leo hii hatakwenda kanisani wala msikitini. Akafanye nini? Watu wake hawako huko! Wakristo na waislamu wanabaki kushikana makoo, "Yesu hakusulubiwa," "Yesu mwana wa Mungu," "Yesu alikuwa ni muislamu," "Yesu alimwaga damu ya ukombozi." Yesu, Yesu, Yesu.... Akija wala hatapoteza muda huko. Atawaacha waendelee na ibada na swala zao na mihadhara na ma-crusade.
 
Kila mara ninaahirisha makala ninayotaka kuandika juu ya hili jambo. Ninahitaji makala ili nichambue vizuri na kufafanua nina maana gani ninaposema kuwa Yesu karibu aondoke. Na kuwa Yesu akitokea Tanzania leo hii hatakwenda kanisani wala msikitini. Watamsikia kwenye "bomba"!

2 Maoni Yako:

At 7/21/2004 04:54:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Naona uandeleza kufuru zako. Shauri yako.

 
At 7/25/2004 07:11:00 AM, Blogger Absalom Kibanda said...

Nimeisikia hii falsafa yako ya kwamba Yesu alishakuja na yuko njiani kuondoka kwa muda mrefu sasa. Nadhani kabla watu hawajapata fursa ya kuchangia unapaswa kutimiza hiyo azma yako ya kuandika makala ya kina ndipo tufahamu iwapo una hoja ya kuutetea mtazamo wako ama la.

Iwapo Yesu alikuwa akisema kwa mafumbo (sote tunakubaliana) basi unapaswa kutambua kwamba huo uteguzi wako wa fumbo waweza ukawa ni ama sahihi au siyo.

Hata hivyo naomba unijibu swali langu moja. Hivi Yesu alikuwa akimaanisha nini aliposema atakaporudi kila jicho litamuona akishuka mawinguni akiwa na utukufu utokao kwa Baba? Iweje basi kurudi kwake mkuone ninyi wachache tu? tena pasipo hata kupitia mawinguni?

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com