7/10/2004

UTANYONYESHA AU...?

Mwanamke akiwa na mimba hapa Marekani, kati ya maswali ambayo atakumbana nayo akienda hospitali ni, "Je una mpango wa kunyonyesha au?" Kama umetokea nchi za ulimwengu unaiotwa wa "tatu" utabaki mdomo wazi. Swali hili alipoulizwa Mama Ukweli nilikuwa nikisema, "Kwani mwanamke aliyejifungua anakuwa na maziwa ya nini?" Maziwa ya mama si kwa ajili ya mtoto? Si ndio kanuni ya maumbile hiyo?

Kumbe nilichokuwa sifahamu ni kuwa nchi zinazodaiwa "kuendelea" ni nchi ambazo hazijali afya ya mtoto. Wanawake wanajali kutunza maumbo ya matiti yao. Hawataki kunyonyesha. Asilimia ya wanawake wanaonyonyesha ni ndogo sana. Kunnyonyesha sio tendo linalofanywa hadharani. Ukinyonyesha hadharani watu watakukudolea macho kama vile hazimo.

Wanyama, ukiacha binadamu, wananyonyesha watoto wao. Binadamu ndio viumbe pekee vinavyoamua kuwapa watoto wao maziwa ya wanyama wengine na sio maziwa yao. Na wakati huo huo tunadai kuwa binadamu tumeendelea kuliko ng'ombe au mbuzi. Mbona wao wana busara zaidi yetu kwa kuwapa watoto wao chakula chao?

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com