7/03/2004

Babu Seya!

Hii habari kuwa watu wanaandamana kutaka serikali imsamehe Babu Seya na watoto wake kutokana na kifungo cha maisha inanitia kichefuchefu kabisa. Yaani wasamehewe kwakuwa ni waimbaji maarufu? Babu Seya angekuwa ni mlalanjaa Mzee Ramazani na wanaye wa Tandale wamehukumiwa kifungo cha maisha watu wangeandamana? Au mtu maarufu akivunja sheria hapaswi kufungwa? Jela ni ya watu masikini na wasiojulikana sio? Acheni kunikosesha hamu ya chakula!

2 Maoni Yako:

At 7/04/2004 09:50:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Wabongo utawaweza? Watu wanapoteza muda wao kuandamana. Sidhani kama viongozi ni wajinga kiasi hicho. Wasamehewe kwa vigezo gani?

 
At 7/05/2004 08:37:00 PM, Anonymous Anonymous said...

wako watu wengi wanapatikana na kosa la kubaka au kunajisi ila hawafungwi kifungo cha maisha. Kwani kosa lao ni kuua?

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com