7/05/2004

Mapinduzi ya Zanzibar eti ni Uhaini!

Leo nilikuwa natembelea tovuti (website) mbalimbali. Mara nikakumbana na hii tovuti ya huyu bwana anayedai kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni uhaini. Na kuwa yote tunayoelezwa juu ya unyama wa utawala wa Waarabu katika kisiwa hiki cha marashi ya karafuu (hivi timu ya KMKM bado iko?) ni uongo mtupu. Habari utaipata ukibonyeza HAPA.

2 Maoni Yako:

At 7/06/2004 08:09:00 AM, Anonymous Anonymous said...

mbona kuna kazi? Ngoja nirudie tena kumsoma huyu bwana. Ila kiswahili chake vipi?

 
At 7/07/2004 03:44:00 AM, Blogger chaurembo said...

Haya, tumesoma yaliyowakuta hawa ma-HizbulWattan. Basi kila mapinduzi kuna wanaofaidika na wanaoteseka. huko Cuba wengi wamikimbilia Miami, huko Urusi na kwengineko wengi walikwenda ulaya ya Magharibi...
Huko Unguja baada ya mapinduzi, kama anavosema mwandishi wengi waliondoka pia... pamoja na maoni na mafunzo ya TANU na AFRO-SHIRAZI na baadaye CCM, itafaa tukumbuke si Karume si Nyerere, hakuna mwanasiasa mwenye sifa za malaika! Na siasa za Unguja na Bara zilijawa uwongo na ukandamizaji wa akili... kumbuka huko bara hata televisheni ilikuwa dhambi, redio kaseti pia... je unakumbuka vita ya wahujumu uchumi?
Hata maongezi nyeti watu hawakuweza kusema.. ati kuna wanaokuona.... Wanamgambo wa JKT walifunga watu mashati na kudai vitambulisho bila kujali utu wa raia. Basi itakuwa kizuizini kukosekane mateso... Ndio Wengi waliuwawa...
Lakini mwisho sijaafikiana na mwandishi kuwa Nyerere ni mpinga Uislamu.Kwamba Mapinduzi yalikusudia kukandamiza Uislamu na sio Uwarabu. Nauliza nionyeshe uzalendo wa Mwarabu ulio ghairi ya Uisilamu.. si palestina si Algeria wala si Sudani. Uwarabu na Udini vimefungatana,
Na juu ya utumwa, kwamba mapiduzi yalitokeshezea muda mrefu baada ya utumwa kusitishwa unguja, na kwamba hapakuwa na matabaka bali dola shwari.. nawaomba mrejee historia ya kusitishwa utumwa..
BWANA NDESANJO, Asalaaim Alaikum

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com