7/10/2004

ugali na mihogo

Leo mchana na usiku nimekula ugali wa nguvu. Kesho au keshokutwa lazima nijichane kwa mihogo. Chakula cha Tanzania ukiwa Ughaibuni kinakuwa na utamu mara mia zaidi. Jamani sisi tuna chakula kizuri sana. Naona kuna watu wanaona ufahari kukimbilia hivi vyakula vya "kuchukua" (take away)au vyakula vya hoteli kubwa, ambavyo majina yake ukitamka unaweza kuvunja jino, wakidhani kuwa ndio moja ya alama za maendeleo. Wapi! Kama unaona kuwa kula ugali wa kisamvu na nazi na parachichi ni kuwa nyuma kimaendeleo, unahitaji dawa ya kutibu ugonjwa ninaozungumzia kila siku: utumwa wa kimawazo. JIKOMBOE!

2 Maoni Yako:

At 7/10/2004 11:35:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Huo ugali unaokula huko sio ugali...unga wa yanga au?

 
At 7/19/2004 04:17:00 PM, Blogger sedia said...

Kumbe...umekula mihogo? Wapi? Nani amepika? Hmmmmmm.
- mke wako

p.s. Thanks "anonymous" for your comments in my blog. That was very sweet. And don't come home pretending it wasn't you because I know how you talk and write (even when you try to disguise it). Sorry for tainting your blog with the English language, by the way.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com