7/18/2004

Shairi: Warsha, mikutano....

SAHAU KABLA YA ALFAJIRI !
La mgambo limelia
wa kusikia wamesikia,
kama ni Ukimwi, haya
kama ni wanawake, haya
kama ni utandawizi, haya
kama ni watoto, haya,
ili mradi una ishu
inayokubalika
kwa wafadhili.
 
Usijali.
 
Mikutano
warsha
makongamano
semina
vikao
utafiti
mafunzo....
 
Tukutane
tuongee
tulalamike
tuonye
tushauri
tukemee
tunywe chai, kahawa
mlo wa mchana
mshiko tushike
picha tupige
tuondoke
tusahau yote kabla ya alfajiri. 
 
Mla kesho ni mla leo.    
                                         - July 18, 2004, Toledo, OH
 

1 Maoni Yako:

At 7/21/2004 04:55:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Acha kuingilia kula ya watu. Bila mikutano tutakula wapi fedha za wafadhili?

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com