7/12/2004

Babu Seya

Itabidi nifanye nifafanue kidogo juu ya mawazo yangu kuhusu suala la Babu Seya. Nimepata barua pepe nyingi. Baadhi zinaonyesha kuwa hoja yangu ya msingi haikueleweka. Nitatoa ufafanuzi baadaye ndani ya blogu hii. Na pengine kwenye makala ya jumapili. Rudi baadaye. Ninakwenda nyumbani kupumzika. Kwahiyo baadaye. Uhuru!

1 Maoni Yako:

At 7/13/2004 02:50:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Hi, brother,
Nimekufahamu kuhusu suala la Babu Seya, ila ushauri wangu ni kwamba tuendelee kusubiri hatma ya rufaa yao, nadhani hii ni busara kidogo.

Kwa sasa nadhani jamii zote za dunia hii zipo au zimekumbwa na misukosuko na machafuko ya kila aina.
Suala la uatandawazi na athari zake kwa jamii masikini kama ilivyo kwa Tanzania! Nadhani hili swala linatisha sana. Hapa kwetu Bongo tunaona jinsi ambavyo mambo mengi yanatendeka kinyume na haki za kimsingi za binadamu kwa kisingizio cha utandawazi: watu kuachishwa kazi, kusimamishwa na upendeleo katika ajira. Hii imesababisha kuwepo na ongezeko kubwa la wimbi la wasio na kazi na hivyo kuongeza maovu katika jamii kama ujambazi, uchangudoa, n.k.
Hao wakubwa zetu huko majuu sijui wana agenda gani kwa nchi changa na suala zima la utandawazi.
AGOA na NEPAD: sijafanikiwa kuona kama ni programu zenye matokeo ya mafanikio sana kwetu. Kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu sasa, AGOA ipo na Tanzania tumeambiwa tumeweza kupeleka bidhaa kidogo sana mamtoni (Marekani), sijui kama wao wameleta kidogo hivyo kwetu!
wakati fulani nikiwa nahudhuria kozi fulani, Profesa mmoja alisema kwa utani kuwa NEPAD ni "knee pad". Lakini najaribu kuona ni kweli, kwani NEPAD yenyewe inatuelekeza zaidi kwenye kuomba-omba kuliko kujitegemea sisi wenyewe. Tutaendelea na hali hii hata lini?
Sasa maono yangu ni kwamba, utandawazi ndo hivyo tunao na hatuwezi kuukwepa, hivyo basi ni vema tukajitahidi kwenda nao sambamba tukichuma faida zake zaidi kuliko kukaa tu na kuacha eti mambo yatajipa! Ha!! tutachekesha!, wenzetu watakuwa wanakimbia sisi tumelala, watafaidi na zaidi wataendelea kutunyonya kwa mamirija makubwa zaidi ya yale yaliyokuwepo.
Tusimame tuiokoe na kuibadili hali hii!! Haya yanaweza yakawa mawazo ya kimapinduzi, ila nionavyo mimi, ni kweli kwamba tunahitaji mapinduzi kataka kila nyanja ya maisha kwa sasa.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com