7/23/2004

Utata wa ndoa Marekani

Wabunge wenye siasa za kihafidhina wameshindwa kupitisha sheria ambayo ingeifanya katiba ibadilishwe ili kutamka kuwa ndoa ni kati ya mwaume na mwanamke! Rais Bush na chama cha Republican wamekuwa mstari wa mbele kutafuta njia ya kuzuia kisheria kasi ya ndoa za wanaume kwa wanaume na wanawake kwa wanawake. Swali ambalo Bush na wenzake wanashindwa kujibu hadi hivi sasa ni hili: kwanini wanataka kubadili katiba kwa kutumia imani zao za kidini?
Bush na wenzake wanadai kuwa ndoa mwanaume na mwanamke ndio mapenzi ya Mungu. Sasa kama je mtu hamwamini huyo Mungu wao? Hili suala kwa kifupi ni gumu sana. Huko Afrika Kusini kipindi cha luninga cha Yizo Yizo kimeonyesha wanaume wawili wakipigana busu kwa mapenzi na mahaba yasiyo na kifani. Ni mara ya kwanza kwa luninga nchini humo kuonyesha picha ya namna hii. Afrika Kusini ndio nchi pekee Afrika hivi sasa ambayo katiba yake inatoa haki kwa watu wa jinsia moja kuwa na mahusiano ya kimapenzi.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com