7/21/2004

Narudia Shairi

Narudia kuweka tena sehemu ya shairi langu liitwalo "Utamaduni Msalabani." Wengi wametaka niweke sehemu nzima. NItafanya hivyo karibuni. NItarudia sehemu niliyoweka mwezi uliopita. Nataka usome na utafakari sana mistari hii michache.

Utamaduni Msalabani
Kura twapiga,
Sadaka twatoa,
Kodi twalipa,
swala twasali,
Walalanjaa Cha moto,
mbona
Bado twakiona?
 
Demokrasia ghasia
Mafukara twauziwa,
Jehanamu ya moto
Masikini twatishiwa,
Wa kusema wamesema
Wa kusikia ni viziwi,
Hivi chukua chako mapema
Ni azimio la wapi?
                                         - Dar Es Salaam, Tanzania 2003

1 Maoni Yako:

At 7/21/2004 05:04:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Kwanini huweki shairi zima?

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com