7/23/2004

Kenya Wanatufundisha Nini?

Baada ya wapinzani kumtoa madarakani dikteta aliyekalia kiti toka mwaka 1979, Mzee Moi, wapinzani wa Tanzania walitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wakatae chama tawala na kuleta mabadiliko. Kama Kenya ndio mfano ambao viongozi wa upinzani Tanzania wanataka wananchi wauige, basi huu ni mfano mbaya sana. Kenya inatupa fundisho moja kubwa sana. Vyama vya siasa vinaongozwa na binadamu. Viwe ni vyama vya upinzania au chama tawala. Wezi wa chama cha KANU hawakuwa wakiiba eti kwakuwa wao ni wanachama wa KANU. Waliiba kwa kuwa ni wanadamu ambao hawana maadili na utu. Ubinadamu wa viongozi wa upinzania hauna tofauti na ubinadamu wa viongozi wa chama tawala. Tunaona jinsi ambavyo viongozi waliokuwa wakidai kuwa katiba ya Kenya ibadilishwe, sasa wameingia madarakani wamebadili msimamo. Tumeona kashfa za rushwa zinawaandama kila kukicha. Leo hii gazeti la Daily Nation lina habari hii ya Waziri wa Uchukuzi ambaye inaelekea kapewa kitu kidogo na Wachina. Umeusikia wimbo wa Wainaina  uitwao Kenya Nchi ya Kitu Kidogo? Anasema, "askari kama unataka chai nenda Limuru: Limiru inalimwa chai. Kenya ni nchi ya kitu kidogo wakati wa "baba" Moi. Ni nchi ya kitu kidogo wakati wa Mzee Kibaki. Halafu unaona nchi zetu za Afrika, badala ya ku-recycle takataka, tuna-recycle watawala.













0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com