7/23/2004

SITAOMBA MSAMAHA...

"Sitaomba msamaha." Haya ni maneno ya Rais wa Ufilipino, mwanamama Gloria Arroyo, kufuatia kuondoa majeshi ya nchi yake toka Iraki ili kuokoa maisha ya Angelo de la Cruz aliyekuwa ameshikiliwa mateka huko Iraki. Arroyo anasema kuwa Angelo ana familia ya watoto tisa wanaomhitaji hivyo uhai wake ndio kipaumbele cha nchi yake. Serikali ya Rais Kichaka (Bush) imetoa malalamiko juu ya hatua hiyo.

Tujiulize: Hivi binti yake Bush angekuwa ameshikiliwa na hao jamaa na wakiwa wanatishia kumkata kichwa, Bush angesema, "Potelea mbali. Wamuue. Siwezi kutimiza masharti ya magaidi. Nafuu mtoto wangu auawe kikatili kuliko kuwasikiliza. " Angethubutu kusema hivyo? Thubutu!


0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com