1/22/2006

Unamjua Spika Wa Wanablogu?

Nimeamka asubuhi hii na kwenda moja kwa moja kwenye ukumbi pepe wa mjadala kuhusu neno muafaka la Kiswahili la teknolojia hii ya blogu. Nikasoma mawazo mazuri sana ya wachangiaji, nami nikaweka neno langu. Napenda uende pale ili ujue mjadala umefikia wapi. Kuna masuala fulani ya kinadharia kuhusu lugha na kuhusu blogu ambayo yamejitokeza. Ila pia mjadala huu umetuletea Spika. Unajua Liberia wamepata rais mwanamke. Ujeremani wamepata Kansela mwanamke. Chile wamepata raisi mwanamke. Tanzania imepata waziri wa fedha mwanamke. Kuna jambo linatokea duniani hivi sasa. Nasi tumepata spika mwanamke. Ukitaka kumjua nenda kwenye ukumbi pepe wa majadiliano ya neno blogu. Spika huyu tumekuwa tukimwita Mheshimiwa ila napendekeza tumwite ndugu. Naona neno ndugu lina maana nzuri zaidi ya mheshimiwa. Watwawala wetu wanaitwa waheshimiwa...si ndio?
Haya, bonyeza hapa.

1 Maoni Yako:

At 1/22/2006 06:38:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Ndiyo Waheshimiwa,

Naandika ujumbe huu huku nikiwa nacheka kwa utamu wa majadiliano yenu.

Nawatakieni kila la heri katika harakati yenu ya kutafuta neno litakalosawiri kiungo hili muhimu kati yetu.

Ni miye maridhiya,
F MtiMkubwa Tungaraza.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com