1/15/2006

Vita ya Msituni Inahamia Kwenye Mtandao Pepe

Jamaa wa gazeti la Washington Post wana habari moja nimeisoma dakika hii kuhusu wapiganaji wa msituni Afrika wanavyotumia zana mpya za mawasiliano (blogu zikiwemo) na pia jinsi ambavyo mtandao wa tarakilishi unavyoweza kusaidia wapinzani wa serikali zenye tabia ya kufungia magazeti na redio. Binafsi nadhani habari hii ni nzuri ila mwandishi hakuifanyia utafiti wa kutosha. Bonyeza hapa uisome.

2 Maoni Yako:

At 1/16/2006 01:37:00 AM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

Blogu ni nyenzo muhimu ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru! viva blogu!

 
At 1/17/2006 05:24:00 AM, Blogger Innocent Kasyate said...

jamaa wa serikali ya TZ kwa mfano wakisikia haya wanachanganyikiwa kabisa.Ndio maana serikali kadhaa zinataka teknolojia ya mtandao imilikiwe na serikali.Mnakumbuka kule
Tunisia?Eti UN isimamie mtandao,nafurahi hawakufanikiwa.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com