1/07/2006

Mkutano wa Podikasiti: podikasiti darasani

Mkutano ndio unafikia mwisho. Umebaki muda wa mvinyo, kujuana zaidi na kubadilisha kadi. Mada tuliyokuwa tukiijadili awali ya matumizi ya podikasiti kufundishia unaweza kuiona kwa kubonyeza hapa. Kiungo nilichotoa hapo chini kinaweza kukupa shida kuipata. Hiki cha sasa kinakupeleka moja kwa moja. Unaweza kuona mfano wa kazi ya watoto wa shule waliyofanya kwa kutumia teknolojia ya podikasiti. Bonyeza hapa.

Kinachofuata sasa ni Jikomboe kupanuka. Kwa sasa Jikomboe, yaani blogu hii, ni kama gazeti pepe langu. Sasa itapanuka kuwa sio gazeti pepe tu bali redio pepe na luninga pepe (podikasiti ya video). Mwambieni Mengi akae chonjo, wanablogu tunaingilia nyanja ya habari kwa ari mpya na nguvu mpya (nakopa maneno yaliyotumika kutufanya tuamini kuwa tunajenga nchi mpya kwa sura zile zile au sura mpya zenye mtazamo kama zile sura za zamani).

Kama tusemavyo kule Moshi ninawaambia, "Watashaa." Kama hujui maana yake muulize Mtafiti.

2 Maoni Yako:

At 1/08/2006 09:52:00 PM, Blogger Better tomorrow said...

Niliwashaambia hata mimi wasipo soma watasikia tu..Jikombe mtandao ulikamilika unakuja kwa nguvu sijui niseme ..( ).
Mahorima yameaamia macha!

 
At 1/09/2006 04:58:00 AM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

pawa sawo mooosha ruwa! aikambe meku! sasa hapo nadhani hii itaongeza nguvu ya kujenga maoni ya kueleweka miongoni mwa watanzania. bwana ndesanjo tuko wote tukikuunga mkono kwa nguvu zote. hapa hata kina bwaya na wengine wetu sasa ni faraja sana. siku moja nilichangia pale kwa mwandani nikasema hivi itakuwaje tukiweka mgomo kususia kununua magazeti yale ya tanzania? yasiyofanya kazi inavyopasika na kujiingiza kwenye upande kisiasa? hili nalo ni jibu.

cheers

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com