Somo, Ngoma, na Tambiko la Kwanzaa
Nikifundisha watoto (unajua tena samaki mkunje angali mbichi) maana ya Kwanzaa na umuhimu wake kwa watu wenye asili ya Afrika. Katika picha nyingine hiyo: huyo ni Barry akifungua somo la Kwanzaa kwa ngoma baada ya kutoa tambiko. Barry ni Mmarekani Mweusi ambaye amejifunza kupiga ngoma aina ya Djembe katika nchi ya Guinea, Afrika Magharibi. Mikono yake migumu kama tairi la nyuma la trekta aina ya Kubota (hivi Makubota yaliishiaga wapi?). Juu ya Kwanzaa soma niliyoandika hapo chini na pia bonyeza hapa.
Bonyeza juu ya picha zenyewe uzione kwa karibu zaidi.
1 Maoni Yako:
Ndesanjo mimi nashukuru huu utaratibu wa kutuwekea vipicha maana vinatuwezesha kuwa karibu na tukio na kufahamiana zaidi. Kazi njema hao ni muhimu kwani zama zao zipo mbele kuliko zetu
Post a Comment
<< Home