1/16/2006

TUMKUMBUKE MARTIN LUTHER KING

Leo ni siku ya kitaifa nchini Marekani ya kumkumbuka mpigania haki za watu weusi na binadamu wote, Dakta Martin Luther King. Ninakupa viungo kadhaa vya hotuba zake ambazo zilikuwa zinasisimua mno kutokana na ufundi wake wa kuhubiri. Bonyeza hapa uone video za hotuba zake. Hapa kuna video ya mahojiano. Bofya hapa kwa mkusanyiko wa video mbalimbali.
Kuna hotuba zake mbili muhimu sana kusikiliza: ya kwanza ni ile ya "Nina Ndoto." Bonyeza hapa usikilize. Hotuba ya pili ni ile ya "Nimefika Kileleni Mlimani" ambayo utaipata ukibonyeza hapa.

1 Maoni Yako:

At 1/16/2006 11:09:00 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Naketi kichuguni,mkononi nimeshika manati yangu,nawinda ndege ili familia isikose kitoweo,halafu najiuliza,taarifa ya habari leo asubuhi imetaja jina la Martin Luther King,hivi alikuwa ni nani hasa,nasikia aliuawa,wapinga maendeleo walimwangusha.Hivi leo hii wangapi wanathamini mchango wake kwa dhati,wakaacha kuishia kusema kwa midomo tu kwamba,leo ni siku ya King?!Hivi hao watu weusi wenyewe,nikiwemo na mimi mara ngapi wanatafakari alichokianzisha Martin Luther King na wala asikimalize,wao/sisi mchango wetu nini?Mbona tunazidi kushindwa?Nini hasa kimebadilika tokea ahutubie kuhusu ndoto yake?Mbona naona kama mambo ni yale yale?Ubaguzi ni ule ule,haki za weusi au binadamu ni mashakani kama enzi zile tu.Nalia,ndio maana unaona kwikwi za kilio katika ninachoandika.Ngoja kwanza,kuna kundi la ndege limetua mbele yangu.Kitoweo kimejileta!

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com