1/16/2006

Blogu ya mwongozo wa jinsi ya kublogu

Kutokana na maswali ninayopata toka kwa watu wenye nia ya kublogu na hamasa kubwa waliyonayo watu wengi wenye kutaka kutumia teknolojia hii kutoa mawazo yao, kujieleza, na kuelimishana na wengine, nimeamua kujenga blogu maalum ya mwongozo kwa wanaotaka kublogu na pia wale ambao tayari wanablogu. Blogu hii itasaidia watu wa kawaida wanaotaka kublogu, itakuwa na eneo la waandishi wa habari wanaotaka kublogu, kutakuwa na ukurasa kwa ajili ya wanaharakati au wenye mashirika yasiyo ya kiserikali wanaotaka kublogu, ukurasa wa kusaidia wanasiasa wanaotaka kublogu, ukurasa wa kusaidia wanaoblogu jinsi ya kutangaza blogu zao, ukurasa wa maelezo kwa wale wanaotaka kublogu bila kujulikana kuwa wao ni akina nani (kwa mfano, kama unafanya ofisi ya rais na unaona mambo ambayo unadhani ni muhimu umma ukajua lakini hutaki rais ajue kuwa wewe ndiye unayetoboa siri!), n.k. Iwapo kuna suala ambalo ungependa liwe na ukurasa wake, usisite kuniambia. Majina ya kurasa zenyewe yako upande wa kuume wa blogu hiyo, chini ya orodha ya miezi. Blogu hiyo utaiona kwa kubonyeza hapa.

5 Maoni Yako:

At 1/16/2006 07:20:00 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Kazi nzuri na muhimu sana hii Ndesanjo.Tupo pamoja.

 
At 1/17/2006 09:08:00 AM, Blogger boniphace said...

Matunda ya jitihada hii yanazaa matunda sasa nina mwingine aliyekuja anaitwa NURU AKILINI waweza pita kwangu na kumpa nafasi hapa kwako pia.

 
At 1/17/2006 11:24:00 PM, Blogger mwandani said...

safi ndesanjo. mpaka tufike mamilioni

 
At 1/19/2006 09:41:00 AM, Blogger Indya Nkya said...

Poa sana angalau jitihada zinazaa matunda. Watu wanaongezeka kwa kasi kublogu hii ni dalili kwamba kazi inakubalika

 
At 1/26/2006 06:15:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Bwana Chris ni vyema apewe shukrani. Anafanya kazi hii bila ujira wowote. Unaweza kumpa shukrani kwa kumtembelea kwenye blogu yake:
www.pictr.org

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com