10/20/2005

Pop!Tech: Mkutano umefikia tamati kwa leo

Watu tunatawanyika kwa leo. Waafrika tuliokaribishwa kwenye mkutano huu tunatakiwa kwenda kula chakula cha usiku na waandaaji. Nimefurahi hawajafanya lile jambo linaloniudhi sana. Unajua kuna hizi sherehe unakribishwa, kisha kwenye kadi wanaandika kuwa unatakiwa kuvaa suti nyeusi. Kama unanikaribisha, nikaribishe sio eti unipangie hadi namna nitakavyovaa. Yaani unakuja hadi kwenye kabati langu la nguo kunichagulia nivae nini?
Sasa mimi nilivyo na kiburi...ingawa siku hizi kimepungua. Kiburi kikipungua wanasema ni dalili ya uzee! Nasema nilivyo na kiburi mimi huvaa kinyume na wanavyotaka. Kwa mfano, kule Helsinki waliponipa ile kadi ya chakula cha usiku na kutaka nivae suti nyeusi...unajua nilivaa nini? Nilivaa kanzu nyeupe ya toka Ghana! Leo naona hawajataka kuleta hii habari ya kutuchagulia nguo. Usinikaribishe hata siku moja na kunipangia nivae nini...unasikia?

Baadaye wandugu. Pop!Tech inaendelea kesho.

3 Maoni Yako:

At 10/21/2005 01:35:00 AM, Blogger Indya Nkya said...

Tuambie vizuri. Kiburi kupungua kunaweza kuwa ni kwamba unakubaliana na mambo ambayo ulikuwa hukubaliani nayo awali. kama ni hivyo basi ni hatari. Walikuruhusu kuingia bila suti nyeusi? kama walikuruhusu basi hakuna maana kumpangia yeyote nguo!

 
At 10/21/2005 08:27:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Nkya, kwa madongo ya chini chini nakuvulia kofia. Lakini umenifurahisha maana inamaanisha kuwa tatizo la kupunguza kiburi sio uzee. Kwahiyo hofu ya uzee naona sasa itanitoka!!!!

 
At 10/21/2005 09:12:00 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Nakubaliana na wewe Ndesanjo kwa asilimia zote.Nimewahi kukataa mialiko mingi yenye masharti ya kipumbavu namna hiyo.Niliona picha zako za Helsinki na kwa kweli nilifurahi.Tupo pamoja katika hilo.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com