6/30/2005

Mahojiano na BBC (Go Digital)

Leo tumekutana na Paul Mason wa kipindi cha BBC kiitwacho Newsnight. Kazungumzia mkutano wetu naye kwenye blogu yake. Pia tumekutana na mwanablogu wa gazeti la The Observer, Rafael Behr. Kwa ujumla leo ilikuwa siku nzuri sana na isitoshe tumeshinda ofisini siku nzima, hakukuwa na harakaharaka za kukimbilia kwenye matreni na mabasi, jambo ambalo tumekuwa tukifanya toka niwasili hapa jumatatu. Baada ya dakika 20 hivi jamaa wa kipindi cha Go Digital cha redio ya BBC atawasili hapa ofisini kufanya mahojiano nami juu ya masuala ya kublogu Afrika na mengine kuhusu teknolojia mpya ya habari na mawasiliano. Muda mfupi uliopita nimetuma makala yangu ya kila wiki katika gazeti la Mwananchi. Makala hiyo, siwezi kuipandisha sasa kutokana na muda kuwa mdogo, nimeipa kichwa hiki: Afrika Itaendelezwa na Waafrika na Kudumazwa na Wazungu.

4 Maoni Yako:

At 6/30/2005 10:08:00 AM, Blogger Indya Nkya said...

Tunaisubiri hiyo makala kwa hamu. Unajua nimetoka sasa hivi kwenye mabishano makali kuhusu Zimbabwe. Nilikuwa nawaaambia jamaa kwamba sisi tunavyowaonea huruma Wazimbabwe kwa hali mbaya iliyopo nchini mwao, wazungu wanaonea huruma makampuni yao yanayowanyonya zaidi hao Wazimbabwe. Kilio chote cha kumondoa Mugabe si ili mzimbabwe wa kawaida afaidi, bali wapate atakayewapa fursa ya kuiba mali asili zao. Hayo ndiyo waafrika wengi wasiyoyaelewa

 
At 6/30/2005 01:52:00 PM, Anonymous Anonymous said...

usiache kuweka hiyo makala. Kuna makala ambazo ulitaja nyuma hujaweka.

 
At 6/30/2005 05:00:00 PM, Anonymous Anonymous said...

I don't understand Swahili but I do recognise dedicated journalists when I meet them! I will see you all in Edinburgh - me and Machreen met Baaba Maal tonight!
Regards, Paul Mason

 
At 7/01/2005 06:19:00 AM, Blogger Maka Patrick Mwasomola said...

Idya Nkya kasema kweli maana hata mimi huwa ninajiuliza kwa nini Zimbabwe tu yaani Blea na Joji wao tuseme Zimbabwe ndo inawauma saana kuliko wazimbabwe wenyewe?Hongera AU kwa kuwaambia wazi kuwa Afrika ina mambo mengi ya muhimu kushughulikia kuliko suala hili la Zimbabwe.Ama kweli wazungu wana visa!

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com